LUTENI Kanali Mstaafu Daniel Gangisa (86) ni mmoja wa mashujaa aliyeoongoza kumng'oa Dikteta Idd Amin Dada katika ardhi ya Tanzania hadi Uganda mwaka 1979.Gangisa ni Mstaafu wa JWTZ ambaye anaishi katika kitongoji cha Chandarua Kata ya Mshangano Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma. Alijiunga na Jeshi la mkoloni mwaka 1947 baadaye mwaka 1950 alikwenda kulinda kisiwa cha Mauritius kilichopo katika Bahari ya Hindi.
Gangisa anasema mwaka 1952 alipelekwa katika kozi ya ukufunzi katika Chuo cha Jeshi cha East African Training Centre kilichopo Nakuru nchini Kenya ambapo katika kozi hiyo alisoma na Dikteta Idd Amin kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 1952 hadi 1954.Anasema Idd Amin alikuwa rafiki yake mkubwa waliishi katika bweni moja na chumba kimoja.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Agosti 3,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa