MAAFISA habari Habari,Mahusiano,Uhusiano na Itifaki serikalini katika Kanda ya Nyanda za Juu wanatarajia kuanza mafunzo ya namna ya kujitangaza kwa kutumia mitandao ya kijamii,Mafunzo hayo ambayo yanaanza leo jijini Mbeya na kumalizika Desemba 19 mwaka huu yameandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Shirika la EQUIP TANZANIA.Kulingana na taarifa ya Rebecca Kwandu kwa niaba ya Katibu Mkuu TAMISEMI,mafunzo hayo maaalum yamelenga kuwajengea uwezo maaafisa hao kutumia mitandao ya kijamii kikamilifu kutangaza shughuli na mafanikio mbalimbali ya serikali ili yaweze kuwafikia wananchi kwa haraka.
Mafunzo yanafanyika kikanda mwezi huu ambapo katika kanda ya Nyanda za juu kusini mikoa inayohusika ni Mbeya,Ruvuma,Songwe.Njombe na Rukwa,Katavi,Kigoma na Iringa.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa