Mafuzo ya Maafisa uchaguzi ngazi ya kata kwa ajili ya uboreshaji wa Daftari la wapiga kura katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma yamefanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo Jaji Msitaafu,ambaye ni Kamishina wa Tume ya Taifa ya uchaguzi kutoka makao makuu Der es salam, Marry Longway amesema Maafisa undikishaji wanatakiwa kuwa makini katika kusikiliza kile ambacho wanafundishwa na wasipo elewa wawewepesi kuuliza maswali.
Jaji Longway, amewaomba kuwa makini sana kwa wale ambao wanaenda kuwaelimisha kwa sababu ndio tume itakayo kuwa inaandikisha na kuburesha upigaji kura pia waelewe wale wenye matatizo tofauti tofauti jinsi ya kuwaelekeza ili wawenze kwenda nao sawa.
“Matumizi ya lugha rafiki ndio jambo la msingi katika kazi yao hata kama ukakutana mtu ambaye hakuelewi jaribu kutafuta njia nzuri ambayo ataweza kukuelewa na msiwe wepesi kukasilika kwa sababu ukikasirika mawasiliano yanaweza kuvunjika na hakuna kitakacho endelea japo changamoto ni nyigi lakini wajitahidi kukabiliana nazo”.Amesema Longway.
Hata hivyo, ametoa rai kusema wajitahidi kuwaonesha tabasamu kwa wale wanao wafundisha ili wameze kuelewana vizuri.
Nae, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Tina Sekambo,amesema wateule hao wameaminiwa na serikali katika kufanya kazi hiyo kwahiyo anawaomba kuwa waadirifu katika kutekeleza majukumu yao naye akiwa kama mwenyekiti.
Vile vile amewataka kuwa makini katika usimamizi wa vyombo ambavyo wamekabidhiwa na Serikali kwa sababu serikali imewaamini katika kusimamia uchaguzi huo kuhusu ulinzi na usalama juu yao wasiwe na wasiwasi.
Pia amesema kuwa na ushirikiano mzuri na tume muda wowote watakapo hitajika wawe tayari kuitikia wito.
Kwa upande wake Afisa uchaguzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Christopher Ngonyani ameyataja malengo ya kuboresha Daftari la wapiga kura ni matu. Kwanza kuandikisha wapiga kura wapya ambao wametimiza umri wa miaka kumi na nane,pili kuboresha taarifa za wapiga kura walio hama sehemu moja kwenda nyingine ili kupata taarifa zao za mwanzo na kuandika upya ili kuondo changamoto za wapigakura kutokujua wapi pakwenda na tatu kurekebishwa na kuondoa wapiga kura walio kosa sifa na kuwaondoa kabisa watu hao ni wenye ugonjwa wa akili ulio thitishwa na daktari
Hata hivyo amesema,baada ya uboreshaji taarifa zote zita bandikwa kwenye mbao za matangazo,na zoezi hilo litaanza tarehe Desembe 30/12/2019 hadi Januari 5,2020.
Imeandikwa na Farida Musa wa Kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa