HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imefanikiwa kupunguza maambukizi ya UKIMWI kutoka asilimia 3.9 mwaka 2017 hadi asilimia 2.7 kufikia Disemba 2018.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Songea Dkt.Mameritha Basike amesema licha ya changamoto zinazoikabili sekta ya Afya katika Manispaa hiyo,elimu dhidi ya UKIMWI imesaidia kupunguza maambukizi ya UKIMWI.
Kulingana na Basike,huduma za Afya ya uzazi na mtoto zinatolewa katika vituo 29 na kwamba Huduma zinazotolewa ni chanjo kwa Watoto chini ya mwaka mmoja, huduma kwa wajawazito na wazazi ili kuzuia maambukizi ya Ukimwi toka kwa Mama kwenda kwa Mtoto ikiwemo ushiriki wa akina Baba.
“Vifo ya Wajawazito bado ni tatizo katika Halmashauri yetu kwani vifo hivyo vimeongezeka toka 188/10000 Mwaka 2016 hadi vifo 202/100,000 mwaka 2018’’,alisema Dkt.Basike.
Hata hivyo amesema jitihada za kupunguza vifo hivyo zimefanyika ikiwa ni pamoja na kukamilika na kuanza kutumika kwa jengo la upasuaji kuanzia Agosti 2017, na kwamba jumla ya akinamama 220 wamepatiwa huduma hii hadi sasa.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa