Wanawake waishio Manispaa ya Songea wakutana na kukubaliana kufanya maandalizi ya siku ya wanawake Duniani ambayo husherehekewa tarehe 08/03/ kila mwaka Duniani kote.
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Songea BI Joyce Mwanja ameawaambia waandishi wa Habari kuwa sherehe hiyo itaadhimishwa kwa kufanya Uzinduzi tarehe 01/03/2020 katika Kata ya Mateka Manispaa ya Songea, na kilele kufanyika 08/03/2020 katika Uwanja wa Majimaji Manispaa songea.
Ametoa rai kwa Wadau mbalimbali Ikiwemo na Taasisi za Serikali, NGO’S, Vyama vya Siasa, pamoja na Vikundi mbali mbali vya akina mama kushiriki katika maonyesho ya Bidhaa na shughuli mbalimbali wanazozifanya kila siku katika kujiongezea kipato.
KAULI MBIU YA MWAKA 2020 NI“ KIZAZI CHA USAWA KWA MAENDELEO YA TANZANIA YA SASA NA BAADAYE.”
IMEANDALIWA NA ;
AMINA PILLY
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa