Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Songea anawatangazia wananchi wote kuwa kutakuwa na huduma ya afya itakayotolewa katika kituo cha Afya Mjimwema na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na Kituo cha Afya Mjimwema.
Madaktari bingwa hao ni wa magonjwa ya meno,macho,magonjwa ya akinamama,magonjwa ya upasuaji,magonjwa ya moyo na kisukari.
Wagonjwa wote wenye uhitaji wa huduma hizo mnatangaziwa kufika katika Kituo cha afya Mjimwema kuanzia Januari 13 hadi 17,2020.Huduma zitatolewa kuanzia saa 2.00 asubuhi.
Hata hivyo kutakuwa na kuchangia gharama kidogo kwa wale wasio na Bima ya NHIF.
Uzinduzi huo unatarajia kufanyika Jumatatu Januari 13,2020 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe. Pololet Mgema.
Kupitia kampeni hiyo wananchi pia watapata fursa ya kupata elimu ya lishe ambayo itatolewa na Afisa Lishe ambaye atatoa mlinganyo wa urefu na uzito wako na atakupa ushauri wa ulaji wa chakula unaofaa ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza.
Afya yako,ndiyo mtaji wako,wote mnakaribishwa
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa