Na,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
11.12.2021
Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema amepokea vyumba vya madarasa 111 leo tarehe 11 Disemba 2021 kutoka katika Halmashauri 3 ambazo ni Halmashauri ya Manispaa ya Songea vyumba vya madarasa 29, Halmashauri ya Wilaya ya Songea vyumba vya madarasa 65 pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Madaba vyumba vya madarasa 17.
Ujenzi wa madarasa hayo ambayo yamekamilika na kukabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Songea, ni utekelezaji wa mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali ya miundombinu ya elimu na afya.
Mgema amewapongeza wakurugenzi na wataalamu wa Halmashauri zote kwa usimamizi bora wa miradi hiyo ambapo hadi sasa ujenzi wa vyumba vyote vya madarasa umekamilika katika viwango vyenye ubora unaotakiwa.
Aliongeza kuwa hadi kufikia tarehe 13 Disemba 2021 shule ambazo bado hawajakamilisha utengenezaji wa viti na meza wanatakiwa kuhakikisha wamekamilisha utengenezaji wa samani hizo ili ifikapo tarehe 15 Disemba 2021 miradi hiyo itakabidhiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.’Mgema Alisisitiza’
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mh.Michael Mbano ametoa wito kwa wataalamu wa Halmashauri zote kuendelea kutumia mfumo wa ujenzi uliotumika kujenga vyumba vya madarasa hayo katika ujenzi wa madarasa mengine ambayo hayapo kwenye mradi huu.
Halmashauri ya Manispaa ya Songea ilipokeaa fedha kiasi cha shilingi milioni 660 ili kutekeleza mradi wa mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa 29.
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa