MADHUMUNI YA KUSAINI MKATABA YA LISHE MANISPAA YA SONGEA
TAREHE 23 OKTOBA 2018
UTANGULIZI
Historia ya kusaini mkataba wa lishe unaanzia tarehe. 19/12/2017 ambapo Waziri wa OR-TAMISEMI Mh. Seleman Jaffo alisaini mkataba wa UTEKELEZAJI MPANGO SHIRIKISHI WA LISHE TAIFA na Wakuu wa Mikoa wote Tanzania bara, na mnamo tarehe 24/09/2018 Mkuu wa Mkoa aliwasainisha Wakuu wa Wilaya wote kufuatia agizo la Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassani alilotoa kwenye mkutano wa urutubishaji chakula uliofanyika Dar es Salaam kuanzia tarehe 23 hadi 24/08/2017. Hii ni katika kuongeza kasi ya utekelezaji na uwajibika katika Swala la Lishe Nchini.
Mkataba huu una malengo matatu,Vipaumbele kumi katika kufikia malengo hayo, Wilaya itakuwa na majukumu na wajibu 17, vigezo 10 vya upimaji utekelezaji wa mkataba na viashiria 10 vya upimaji utendaji kazi. Aidha Mkoa utakuwa na majukumu na wajibu saba katika upimaji utendaji kazi wa wilaya. Haya yote yameainishwa kwenye Mkataba huo.
Mkataba huu utakuwa wa muda wa miaka minne na utaanza tarehe 01 Julai, 2018 hadi tarehe 30 Juni, 2021. Aidha, Mkataba huu utapimwa kila mwisho wa mwaka husika.
Vipaumbele kumi ili wilaya iweze kufikia malengo yaliyoainishwa katika Mkataba huu:-
Ili wilaya iweze kutekeleza malengo hayo ina majukumu na wajibu kumi na saba kama ifuatavyo:
Kutenga fedha kwa ajili ya afua za lishe kama itakavyokuwa inaelekezwa katika mwongozo wa bajeti wa kila mwaka;
Kusimamia ajira kwa wataalam wa lishe katika Halmashauri;
Kusimamia uundwaji wa Kamati za Lishe za Halmashauri kwa mujibu wa Mwongozo uliopo na Kuhakikisha kamati za Maendeleo za Kata na Vijiji/Mitaa zinasimamia maswala ya lishe katika ngazi zao;
Kuhakikisha Kamati za Lishe za Halmashauri zinafanya vikao na kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Mwongozo;
Kusimamia na kuhakikisha sekta mtambuka zinapanga na kutekeleza afua za lishe;
Kuhakikisha kuwa Halmashauri inakuwa na Mpango Mkakati wa Lishe;
Kuhakikisha kwamba mipango ya wadau wote wa lishe inajumuishwa katika mipango ya Halmashauri (MTEFs);
Kuhakikisha kwamba masuala ya lishe yanakuwa ajenda ya kudumu kwenye vikao vyote vya kisheria katika ngazi za Halmashauri, Kata na Vijiji/Mitaa;
Kuhakikisha kwamba, taarifa za kadi alama ya lishe (Nutrition Score Card) inajadiliwa kila robo kabla ya kuwasilishwa katika ngazi husika/inayofuata na pia kutoa mrejesho na kuweka mikakati;
Kujadiliana na kutia saini Mkataba wa Utendaji Kazi;
Kuweka mazingira wezeshi ili watumishi waweze kutenda kazi zao kwa utaalamu, umakini na ufanisi ili kuchangia ipasavyo katika utekelezaji wa malengo ya Wilaya;
Kusimamia utendaji wa kila siku ili kutekeleza Sera, Mikakati na Vipaumbele vya kitaifa kulingana na Mpango jumuishi wa Lishe wa Taifa;
Kuainisha na kuwasilisha changamoto za kiutendaji zinazoikabili Wilaya na kupendekeza mikakati ya kutatua changamoto hizo katika Mamlaka zinazohusika;
Kufanya mapitio ya utendaji kazi wa Wilaya kadiri itakavyohitajika katika kutekeleza Mpango jumuishi wa Lishe wa Taifa;
Kuandaa na kuwasilisha taarifa za utendaji kazi katika Mamlaka zinazostahili kadiri itakavyohitajika kwa muda ulioainishwa;
Kufanya tathmini binafsi ya utekelezaji wa Mkataba wa Utendaji Kazi wa Wilaya kila mwisho wa mwaka na kuwasilisha taarifa katika Mamlaka zinazostahili; na
Kushiriki katika tathmini ya utekelezaji wa Mkataba wa Utendaji Kazi wa Wilaya itakayofanywa na MKOA kila mwisho wa Mwaka.
Katika upimaji wa utendaji kazi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itakuwa na majukumu na wajibu saba kama ifuatavyo: -
Wilaya itawasilisha taarifa za utendaji kazi za robo mwaka na mwaka Mkoani kabla ya tarehe 15 ya mwezi unaofuata, Aidha Iwapo utajitokeza mgogoro wowote katika utekelezaji wa mkataba huu basi pande zote mbili zitakaa pamoja ili kutatua mgogoro huo.
ASANTENI
MKURUGENZI WA
MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa