Madiwani kutoka Manispaa ya Lindi Mjini wamefanya ziara ya siku tatu ya kutembelea miradi mbalimbali Manispaa ya Songea kwa lengo la kujifunza namna wanavyoweza kufikia lengo la kiutendaji.
Akizungumza Mstahiki Meya Manispaa ya Lindi Frank Magari, alisema lengo la ziara hiyo ni kuja kujifunza namna ya uendeshaji wa machinjio ya kisasa ya nyama ya ng'ombe, ujenzi wa shule ya English medium iliyojengwa kwa fedha za mapato ya ndani, usimamizi wa fedha za mikopo ya asilimia 10% na standi kuu ya mabasi Songea, pamoja na namna ya uendeshaji wa vikao vya baraza la madiwani kwa muda mfupi.
Ziara hiyo imefanyika kuanzia tarehe 20 disemba hadi 23 disemba 2023.
IMEANDALIWA NA
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa