MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamepitisha bajeti ya mapato na matumizi kwa mwaka 2018/2019 ambapo imekadiria kutumia zaidi ya shilingi bilioni 57.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Mhandisi Samwel Sanya anautaja mchanganuo wa makisio hayo kuwa ni vyanzo vya ndani vya Halmashauri ni zaidi ya bilioni 3.2,mishahara zaidi ya bilioni 37.76,ruzuku ya matumizi mengineyo zaidi ya bilioni 3.45,ruzuku ya fedha ya miradi ya maendeleo ni zaidi ya bilioni 13.2 na nguvu za wananchi ni milioni 175.
Mhandisi Sanya anabainisha kuwa katika uandaaji wa Mpango wa bajeti katika mwaka ujao,Halmashauri imezingatia miongozi na maelekezo mbalimbali ya serikali ikiwemo Muongozo wa uandaaji wa mpango wa bajeti kwa mwaka 2018/2018.
“Pia tumezingatia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,Hotuba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Hotuba ya Waziri Mkuu na ziara yake ya kuanzia Januari 4 hadi nane 2018 mkoani Ruvuma,Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUKUTA) na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na viongozi ngazi ya Wilaya na Mkoa’’,anasema Mhandisi Sanya.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa