BARAZA la Madiwani la Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma limewachagua wenyeviti wake wapya watano watakaongoza kamati katika kipindi cha kuanzia mwaka mpya wa fedha wa 2018/2019.
Waliochaguliwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uongozi ni Alhaj Abdul Hassan Mshaweji ambaye pia ni Mstahiki Meya.
Wengine ni Osmundi Kapinga ambaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi,Afya,Huduma za Jamii na Elimu na Golden Sanga amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji,Mazingira na Ujenzi.
Wenyeviti wengine waliochaguliwa ni Wilbert Mahundi ambaye anaongoza Kamati ya Maadili na Judith Mbogoro ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Songea anaongoza Kamati Shirikishi ya Kudhibiti UKIMWI.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Agosti 4,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa