Katibu tawala wilaya ya Songea Mtella Mwampamba amewahimiza Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata na mitaa amewataka kuwa makini katika kusimamia suala la uchaguzi ili kufanikisha zoezi hilo.
Mwampamba ameyasema hayo katika mafunzo ya wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata na mitaa yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya Wasichana Songea uliofanyika tarehe 30 septemba 2024 ambao umehudhuriwa na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata na Mitaa kwa lengo la kuwapa mafunzo ya usimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
Kwa upande wake Msimamizi wa uchaguzi serikali za mitaa Manispaa ya Songea mwaka 2024 Wakili. Bashir Muhoja amewataka washiriki wa mafunzo hayo kufuata sheria, kanuni na taratibu za Uchaguzi zilizowekwa.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa