FFARS ( Facility Financial Account and Report System ) ni Mfumo wa Uhasibu na Utoaji taarifa za Fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma, ambao unasaidia kuleta Uwazi na Uwajibikaji na unawezesha utoaji wa taarifa za mapokezi ya fedha, matumizi, na malipo mbalimbali yaliyofanyika kwa kuzingatia sheria na taratibu za manunuzi.
Mfumo wa FFARS unasaidia kufahamu kiasi cha fedha kilichopokelewa, chanzo cha fedha na namna fedha hizo zitakavyotumika katika kufikia lengo lililowekwa la mradi husika ambao unajikita katika utunzaji wa vyanzo vya fedha, kwa kutoa taarifa sahihi ya fedha zote zinazoingia na zinavyotumika.
Mfumo wa FFARS unasaidia kuweka mazingira mazuri kwa wananchi kwa kuwajengea Imani kwa taasis na Serikali yao kwakuwa inawezesha kufanikiwa kwa kutoa maamuzi sahihi ya matumizi ya fedha za miradi inayotekelezwa ngazi ya jamii.
Katika kufanikisha utekelezaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo ngazi ya kata, na Mitaa, Halmashauri ya Manispaa ya Songea inaendelea kutoa mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa FFARS kwa Maafisa watendaji wa Kata na Mitaa yanayofanyika kwa muda wa siku 2 kuanzia tarehe 21/09 – 22/09/2022 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea yanayoendeshwa na wataalam wa TEHAMA.
Afisa TEHAMA Manispaa ya Songea Mvano Mbalale amewataka Maafisa Watendaji wa Mitaa na Kata kutumia Mfumo wa FFARS ambao unasaidia kutoa picha kamili ya kiasi cha fedha kilichopokelewa na unahakikisha kuwa fedha zinadhibitiwa vyema sambamba matumizi sahihi yaliyokusudiwa katika mradi husika.
Aliongeza kuwa Mfumo wa FFARS umetengenezwa ili kusaidia kutoa majibu sahihi ya mahitaji ya fedha kupitia Mfumo ulioboreshwa katika taasisi au watoa huduma ambao wamekuwa wakitumia mifumo hiyo ambayo imekuwa muhimu katika kutekeleza miradi ngazi ya jamii tofauti na mfumo uliokuwa ukitumika hapo awali
Washiriki wa mafunzo hayo wamesema kuwa wanaipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuwajengea uwezo wa matumizi sahihi ya Mfumo wa uhasibu na utoaji wa taarifa za fedha FFARS ambao utawasaidia kufanya kazi kwa weredi mkubwa na kuondoa mianya ya Rushwa katika mazingira ya kazi. “Walipongeza”
Imeandaliwa na
AMINA PILLY
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa