MAFUNZO ya MFumo wa utoaji taarifa katika shule msingi(SIS) yaliyowashirikisha washiriki zaidi ya 300 kutoka Halmashauri zote nane za mkoa wa Ruvuma yamefanyika kwa siku mbili kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya wasichana Songea(Songea Girls) mjini Songea.Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Shirika la TUSOME PAMOJA kwa ufadhili wa USAID ya Marekani kwa kushirikiana na TAMISEMI yamewashirikisha maafisa elimu kata zote,maafisa elimu,maafisa TEHAMA, maafisa takwimu,maafisa uchumi na wathibiti ubora toka Halmashauri zote za mkoa wa Ruvuma.
Mafunzo hayo yamelenga kuwajenga uwezo wa kutumia mfumo wa ukusanyaji wa taarifa za shule za msingi kwa kutumia vishikwambi(Tablets). Mfumo wa SIS ni nyenzo ya usimamizi wa shule na kiini cha taarifa za shule na kwamba SIS inatoa taarifa kwa muhtasari na kwa kina kuhusu utendaji wa shule.
Takwimu ambazo zinapatikana kwenye mfumo wa SIS zinaweza kutumika kusaidia katika kufanya maamuzi na kutengeneza sera,kutoa taarifa kuhusiana na hali ya mfumo wa elimu nchini,kubainisha mahitaji ya kielimu na kusaidia Mamlaka kufanya maamuzi ya namna bora ya kugawanya rasilimali.
Mafunzo ya mfumo wa SIS ngazi ya Halmashauri zote katika Mkoa wa Ruvuma yanatarajiwa kushirikisha walimu wakuu wote na kufanyika kwa siku mbili ambapo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mafunzo hayo yatahusisha walimu wakuu 75.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Juni 6,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa