Mwongozo wa Mpango na Bajeti ni nyenzo ya kuandaa na kutekeleza Bajeti ya Serikali na taasisi zake pamoja na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka mmoja mmoja, ambao unatoa maelekezo mahsusi kwa maafisa masuuli juu ya ukusanyaji wa mapato na usimamizi mzuri wa matumizi ya fedha za umma ambao unatoa ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa kuzingatia maoteo ya vyanzo vyote vya mapato ya ndani na nje.
Hayo yametamkwa na Mchumi wa Manispaa ya Songea Andambike B. Kyomo wakati wa kutoa mafunzo kwa Wakuu wa Idara na vitengo kwa lengo la kuwajengea uelewa wataalamu hao namna ya uandaaji wa mpango na bajeti wa Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/2021 na 2021/2022 yanayoendeshwa na ofisi ya Mchumi wa Manispaa ambayo yataendelea kutolewa kwa muda wa siku tatu kuanzia leo 18 hadi 20 novemba 2020, katika ukumbi wa SACCOS ya Watumishi wa Manispaa ya Songea.
Kyomo alisema” Mpango ni mchakato wa pamoja wa uandaaji taarifa wenye dira na lengo linalokusudiwa katika kiwango Fulani na bajeti nimakadirio ya mapato na matumizi ya fedha, ili kuhakikisha mpango unafanikiwa kwa wakati uliotarajiwa.”
Madhumuni ya Mwongozo wa Mpango na Bajeti wa mwaka ni pamoja na Kuhakikisha ufanisi katika utayarishaji wa Mipango na Bajeti, Kuainisha vipaumbele vya Serikali vitakavyozingatiwa katika bajeti, pamoja na Kutoa maelekezo mahususi ya Serikali kwa Maafisa Masuuli watakayopaswa kuyafuata kwenye Mipango na Bajeti za mafungu yao. Kyomo alibainisha.
Aliongeza kuwa kila mpango na Bajeti wa Serikali lazima uzingatie vipaumbele muhimu vinavyogusa jamii ikiwemo Kukuza Uchumi na Maendeleo ya Viwanda, Kusimamia na kuendeleza Mipango Miji na Makazi, Maendeleo ya Watu ambayo ni hatua za kimkakati katika maendeleo ya watu zinazolenga kuboresha mifumo ya upatikanaji wa huduma za jamii kama elimu, Afya na Ustawi wa Jamii, Maji Safi na Salama, Majitaka, pamoja na uwezeshaji Wananchi Kiuchumi pamoja na miundombinu.
Mwisho, aliwaasa Wataalamu hao kusoma Ilani ya Chama Cha Mapinduzi mara kwa mara ili wanapoandaa mpango na bajeti wa mwaka husika lazima uendane na ilani ya Chama Cha Mapinduzi kujua nini kimeelekeza. “Alisisitiza “
IMETAYARISHWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
18.11.2020
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa