SERIKALI ya Watu wa Marekani imenunua magari sita yenye thamani ya Dola za Marekani 192,000 kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Mwitikio wa Kudhibiti UKIMWI katika mikoa mitano ya Nyanda za Juu Kusini ambayo ni Ruvuma,Mbeya,Katavi,Songwe na Rukwa.
Hafla ya kukabidhi magari hayo toka Serikali ya Marekani imefanyika katika viwanja vya bustani ya Manispaa ya Songea,mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vjana,Ajira na Wenyeulemavu Jenista Mhagama.
Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Kaimu Balozi wa Marekani Dkt.Inmi Patterson,Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt.Leonard Maboko,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme na waratibu wa kuthibiti UKIMWI wa mikoa mitano.
Akizungumza kabla ya kukabidhi magari hayo,Kaimu Balozi wa Marekani Dkt.Inmi Patterson amesema kati ya magari sita yalionunuliwa magari matano yanapelekwa katika mikoa mitano na gari moja linabaki makao makuu ya TACAIDS kwa ajili ya ufuatiliaji na usimamizi.
Naye Mgeni rasmi katika hafla hiyo,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana ,Ajira na Wenyeulemavu Jenista Mhagama akizungumza kabla ya kukabidhi magari hayo kwa waratibu wa kudhibiti UKIMWI katika mikoa mikoa mitano,ambayo wanatekeleza mradi katika maeneo ya kinga,matunzo,matibabu na kupunguza athari zinazotokana na UKIMWI amewaagiza kuhakikisha wanafanyakazi kwa tija na ufanisi wa hali ya juu.
Ugonjwa wa UKIMWI umekuwepo Tanzania kwa takribani sasa Zaidi ya miaka 30,kulingana na utafiti mikoa mitano ya Nyanda za Juu Kusini imekuwa na viwango vya maambukizi vya juu ya wastani wa viwango vya kitaifa ambao ni asilimia 4.7.
Katika utafiti wa mwaka 2016/2017 wa viashiria vya maambukizi ya virusi vya UKIMWI,takwimu zinaonesha kuwa Mkoa wa Mbeya maambukizi ni asilimia 9.3,Katavi asilimia 5.9,Rukwa asilimia 4.4,Ruvuma ni asilimia 5.6 na Mkoa wa Songwe ni 5.8,Kutokana na takwimu hizo.ni wazi kuna umuhimu wa uwepo wa mradi wa usimamizi na ufuatiliaji wa muitikio katika ngazi za vijiji,mitaa na kata katika mikoa hiyo mitano ya Nyanda za Juu Kusini ambayo maambukizi yanazidi wastani wa kitaifa ambao ni asilimia 4.7.
Mwandishi ni Albano Midelo
Afisa Habari wa Manispaa ya Songea
Mawasiliano yake ni albano.midelo@gmail.com,simu 0784765917
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa