Yusta Antoni Mkazi wa Namanditi Kata ya Ruhuwiko Halmashairi ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma amefanikiwa kuwasomesha watoto wake hadi chuo kikuu kutokana na kufanya biashara ya maharage pori maarufu kwa jina la mangatongo ambapo amesema amekuwa anauza mangatongo ambayo yanamuingizia kati ya shilingi 15,000 hadi 20,000 kwa siku na kwamba kupitia biashara hiyo ameweza kumsomesha mtoto wake wa kwanza sekondari hadi chuo kikuu ambapo hivi sasa ni Mwalimu ambaye anafundisha katika Mkoa wa Tanga.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa