Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema kuanzia Novemba 2019 makaa ya mawe ya mgodi wa Ngaka wilayani Mbinga yataanza kusafirishwa na kuuzwa nchini India ambako yatatumika kuendeshea viwanda katika nchi hiyo.
Mgodi wa madini ya Makaa ya mawe wa Ngaka uliopo katika kijiji cha Ntunduwaro kata ya Raunda wilayani Mbinga Mkoani Ruvuma,utafiti umebaini kuwa makaa hayo yanaongoza kwa ubora Duniani.
Kabla ya kuanza rasmi mgodi huo utafiti ulifanyika mwaka 2008 ambapo kiasi cha zaidi ya tani 1000 zilichukuliwa na kusafirishwa kupelekewa nchini Afrika ya kusini kwa uchunguzi na kwamba uchimbaji rasmi ulianza mwaka 2011.
Matokeo yalionesha kuwa madini ya makaa ya mawe ya mgodi wa Ngaka ubora wake haufanani na makaa ya mawe unaochimbwa katika nchi yeyote duniani na kufanya makaa hayo kuwa adimu Duniani.
Mgodi wa madini ya Makaa ya mawe wa Ngaka, unamilikiwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania yenye asilimia 30, na kampuni ya Intra Energy ya Australia yenye Hisa ya asilimia 70
Utafiti umebaini kuwa mgodi wa madini ya makaa ya mawe Ngaka unakadiriwa kuwa na zaidi ya tani milioni 400 za makaa ya mawe,kiasi hicho, kwa mujibu wa wataalam, kinaweza kuchimbwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 100.
.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa