Halmashauri ya Manispaa ya Songea imeendesha zoezi la kukabidhi nyaraka za mikataba na kuanza kwa huduma za usimamizi na ujenzi wa barabara za mjini za kiwango cha Lami nzito katikati ya mji, ambapo kazi imeanza leo tarehe 23 Oktoba 2023 ambayo itafanyika kwa muda wa miezi 18, ambapo miongoni mwa kata zitakazo nufaika na mradi huo ni kata y Mjini, Mfaranyaki, Majengo, na Misufini.
Akizungumza Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya China Sichuan International Cooperation CO,Ltd Tan Jian amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika kufanikisha utekelezaji wa mradi wa barabara ambao umeanza kutekelezwa kuanzia leo tarehe 23 oktoba.
Kwa wa wananchi wameahidi kutoa ushirikiano katika hatua mbalimbali za ujenzi wa mradi huo.
Imeandaliwa na;
Amina pilly
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa