MANISPAA YA SONGEA YA YAPITISHA BAJETI YA ZAIDI YA BILIONI 50
MADIWANI wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea wamepitisha makadirio ya bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 50 katika mwaka wa fedha wa 2020/2021.
Makadirio ya bajeti hiyo yamefanyika katika Kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti Alhaj Abdul Hassan Mshaweji na kufanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye ni Mstahiki Meya Mshaweji amesema makadirio ya awali kwa mwaka wa fedha za 2020/2021 yalikuwa ni shilingi milioni 50,595,932,264.50 ambayo yalitarajiwa kukusanywa kutoka vyanzo mbalimbali vtya mapato.
Hata hivyo amesema makisio hayo yalikuwa ni sawa na ongezeko la shilingi milioni 14,809,745,579.5 sawa na asilimia 41.3 ya lengo la makusanyo kwa mwaka 2019/2020.
“Baada ya mapendekezo ya kuongeza bajeti ya mapato kutoka katika Kamati mbalimbali za kudumu,makadirio ya bajeti yameongezeka kutoka milioni 50,595.932.264.50 hadi kufikia milioni 50,879,671,367.00 ikiwa ni ongezeko la shilingi 283,739,100.00 sawa na asilimia 0.56 ya makadirio ya awali ya mwaka 2020/2021’’,alisema.
Hata hivyo Mshaweji amesema kipaumbele katika bajeti hiyo mwaka huu kimewekwa kwa asilimia 40 katika masuala ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu kujenga miundombinu ya shule na madawati na kukamilisha zahanati kwa ajili ya huduma za afya katika mitaa ya Manispaa ya Songea.
Kwa mujibu wa Mstahiki Meya kipaumbele katika bajeti ijayo pia kimewekwa katika mikopo kwa wajasiriamali wadogo ambao ni wanawake,vijana na wenye ulemavu.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Mkoa wa Ruvuma
Januari 24,2020
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa