“MWANAMKE KATIKA UONGOZI CHACHU KUFIKIA DUNIA YENYE USAWA”
Ni kauli mbiu yenye ukweli usiopingika hapo awali wanawake hawakuhamasika na kushika nafasi za uongozi katika miaka 1990, wanawake katika kaya walikuwa wanafanya kazi nyingi, ujira kidogo, na unyanyasaji uliokithiri, wanawake kutopewa kipaumbele kulinganishwa na wanaume.
Hayo yalibainishwa katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 01 machi 2021 iliyofanyika katika uwanja wa Majimaji Manispaa ya Songea kuelekea siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo 08 machi ambapo kimkoa yatafanyika Wilayani Tunduru.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Mama Askofu wa Kanisa la REDEEMED Songea Mjini Gilda Simon Siluimba ambaye alisema “ Kauli mbiu hii imeandikwa kwa maana ya pekee inawezekana alikuta wanawake ambao bado hawajitambui kama wao ni akina nani,” hivyo alichukua nafasi hiyo kuwaeleza wanawake kuwa nilazima mwanamke ujitambue, ujiamini, alafu uone unaweza”.
Mama Askofu Siluimba alisema Kauli mbiu hiyo inakutambulisha wewe mwanamke ambaye pengine umekata tamaa na kujiona pengine huwezi kufanya jambo lolote, kupitia maadhimisho haya ni lazima tutambue kuwa mwanamke chachu inaamanisha kuwa popote alipo mwanamke mwenye kujitambua lazima jambo liende vizuri, lazima shughuli zisogee na kwa ufanisi mkubwa, pia lazima jambo litaeleweka.
Alisema Tunaishukuru Serikali yetu kwa kutambua nafasi ya mwanamke katika jamii haijalishi kipindi cha nyuma mwanamke hakushiriki kwa usawa kama ilivyo sasa kutokana na Serikali yetu kutambua nafasi ya mwanamke katika jamii imesaidia kwa kiasi kikubwa wanawake hao kupata nafasi za uongozi mbalimbali katika jamii, kushiriki katika maendeleo, pamoja na fursa ya mikopo kupitia vikundi vya wanawake, mikopo inayotolewa na Serikali kupitia Maendeleo ya jamii.
Akinukuu Vitabu vya mungu /Maandiko yasemayo “ Alianza kuumbwa mwanaume au kwa namna nyingine tunasema mwanaume ni TOLEO LA KWANZA na mwanamke TOLEO LA PILI, kwasababu maandiko hayo yameeleza bayana kuwa alitolewa ubavuni mwa mwanaume ili kufanywa kuwa mwanamke kwa hiyo mwanamke ni toleo la pili na kubarikiwa kupewa uwezo mkubwa wa ufahamu wa kufanya mambo mengi kwa wakati, utaalamu mwingi, na akili nyingi na ni nguzo katika familia.”
Amewataka wanawake wote kuishi kwa kujitambua kwani mwanamke chachu katika familia, chachu katika Serikali, chachu katika Ofisi, Chachu kwenye jamii, chachu katika maendeleo, hivyo ni ukweli usiopingika kuwa wanamke ni chachu na ili uwe chachu lazima ujitambue.
Akitoa angalizo kwa wanawake ambao bado hawajitambui kuwa yawezekana ukaitwa chachu kumbe mwenyewe hujitambui na ukawa bado unaishi kama TOLEO LA KWANZA.
Naye Mratibu wa Maadhisho ya siku ya wanawake Duniani Joyce Mwanja alisema lengo la maadhimisho hayo ni kutoa fursa ya kuelimisha jamii hasa wanawake kuhusu jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali, Asasi za Kiraia, Sekta binafsi na wadau wengine katika kukuza hali ya wanawake wa kitanzania pamoja na kupata fursa ya kubainisha upungufu na mbinu za utatuzi wa changamoto zinazowakabili wananwake.
Mwanja alisema Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Afya, Wazee, Jinsia na watoto inayotukumbusha kuendelea kujitambua katika nafasi zao na kuendeleza jamii. Alisema Wanawake wa Manispaa ya Songea wanatoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya tano kwa kuongeza nguvu ya kuwajengea uwezo wanawake kwa kuendeleza jitihada na kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia mfuko wa wanawake, vijana na walemavu ambapo katika kipindi cha mwaka 2020/2021 julai hadi disemba Manispaa ya Songea imekopesha jumla ya Tsh 108,669,444.80 ambazo ziligawiwa kwa vikundi vya wanawake, vijana, na walemavu.
Kilele cha maadhimisho hayo kitafanyika Kimkoa Wilayani Tunduru mnamo 08 machi 2021.
KAULI MBIU; “WANAWAKE KATIKA UONGOZI CHACHU KUFIKIA DUNIA YENYE USAWA”
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
01 machi 2021
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa