MKUU wa wilaya ya Songea Pololet Mgema amesema Halmashauri ya Manispaa ya Songea ina upungufu wa vyumba vya madarasa 500 katika shule za msingi na vyumba 72 katika shule za sekondari.
Kutoka na hali hiyo amewaasa madiwani wa Manispaa ya Songea kusimamia mapato na kubuni vyanzo vipya vya mapato ambavyo vitasaidia kupata fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na huduma nyingine .
Mpango wa elimu bure kuanzia shule za msingi na sekondari kidato cha nne kumechangia uwepo wa idadi kubwa ya wanafunzi ambayo imesababisha changamoto katika vyumba vya madarasa hali inayosabisha baadhi ya wanafunzi kusomea nje.
Katika kukabiliana na hali hiyo watanzania wamekuwa na maoni tofauti ambapo baadhi wameshauri kuundiwa mpango mkakati ambao utawezesha kumaliza tatizo hilo la upungufu wa vyumba vya madarasa kwa sababu kila mkoa tumeshuhudia wingi wa wanafunzi katika shule mbalimbali za msingi na sekondari.
Baadhi ya wananchi wameshauri kuunda Tume itakuwa njia mojawapo nzuri ya kuweza kuziwezesha shule ambazo hazina vyumba vya Madarasa na itawafanya wanafunzi wajisomee kwa amani na kuongeza bidii zaidi ya katika tendo la kujifunza.
Hata hivyo wameshauri tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa serkali kuangalia kwa jicho la tatu hasa katika shule zilizopo vijijini kwa kuwa shule hizo zina changamoto kubwa hivyo Serikali iweke Mipango dhabiti ya mikakati kama ilivyofanya kwenye madawati ili kumaliza tatizo hili.
Ili kumtokomeza adui ujinga mazingira safi ya kusomea ni jambo muhimu ni matumaini yangu kuwa serikali inayoongoza na Rais Dk.John Magufuli kama ilivyofanikiwa kumaliza tatizo la madawati,pia itafanikiwa kumaliza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa nchini.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa