MADIWANI wa Manispaa ya Lichinga nchini Msumbiji mwezi huu wanatarajia kufanya ziara ya mafunzo ya siku sita katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Kulingana na taarifa kutoka nchini Msumbiji ambayo imetumwa kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea,,ziara hiyo inaanzia Agosti 6 hadi 11 na kwamba ugeni kutoka Manispaa ya Lichinga nchini Msumbiji utakuwa na watu 15 ukiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Luis Antonio,Saide Jumo.
"Tukiwa katika Manispaa ya Songea tunatarjia kubadilishana mawazo katika masuala ya mipango na mahusiano,utawala,fedha,mapato,kodi,ujenzi wa miundombinu,usafi na mazingira,usafiri na mawasiliano,utamaduni ,michezo na ustawi wa jamii,'',imesema taarifa ya Mstahiki Meya wa Lichinga.
Hii ni mara ya kwanza kwa Manispaa ya Lichinga kufanya ziara ya mafunzo katika Manispaa ya Songea tangu kuingia madarakani kwa serikali ya Awamu ya Tano inayoongizwa na Rais Dkt.John Magufuli ya HAPA KAZI TU.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Serikalini Manispaa ya Songea
Agosti 5,2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa