HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma inaendelea kufanya maandalizi ya maonesho nan sherehe za NaneNane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ambazo zinaanza Agosti Mosi hadi Nane mwaka 2018.Sherehe hizo zinafanyika katika uwanja wa Maonesho wa John Mwakangale jijini Mbeya.Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Zawadi Nguaro anasema maandalizi ya maonesho hayo yanaendelea vizuri ambapo katika Banda la Maonesho la Manispaa ya Songea ambalo lipo katika viwanja vya maonesho na Nane Nane jijini Mbeya,zimeoteshwa mbogamboga ambazo zimestawi vizuri kama zinavyoonekana katika picha na kwamba zinatarajiwa kuuzwa katika wiki ya kilele cha maonesho ya nane jijini Mbeya.
Kauli Mbiu ya Maonesho ya Nane Nane mwaka 2018 ni WEKEZA KATIKA KILIMO,UFUGAJI NA UVUVI KWA MAENDELEO YA VIWANDA.Maonesho ya mwaka huu yatashirikisha Kampuni,Taasisi za Umma,Taasisi Binafsi na watu binafsi.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Julai 3,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa