KILA mwaka kuanzia Agosti Mosi hadi nane huadhimishwa wiki ya maonesho na sherehe za Nanenane (Sikukuu ya wakulima) ambazo hufanyika ngazi ya Mkoa na Kanda.Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kila mwaka ushiriki maonesho ya Nanenane ngazi ya Mkoa ambayo hufanyika katika viwanja vya Msamala mjini Songea.
Manispaa ya Songea pia kila mwaka ushiriki katika maonesho ya Kanda ambayo hufanyika kila mwaka katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Zawadi Nguaro analitaja lengo la maonesho hayo ya kila mwaka kuwa ni kuwakutanisha wakulima,wajasiriamali,wafugaji,wavuvi,Taasisi binafsi,watu binafsi,kampuni na mashirika.
“Wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo,mifugo na uvuvi watashiriki katika maonesho hayo ili kupata elimu mbalimbali ya uzalishaji bora,ubunifu,upatikanaji wa masoko kwa bidhaa zinazozalishwa’’amesema Nguaro.Ameongeza kuwa wadau hao wakiwa katika wiki ya sherehe hizo,watajifunza matumizi ya teknolojia za kisasa katika uzalishaji ili kuongeza mnyororo wa thamani kwa mazao ya kilimo,mifugo na uvuvi.
“Ukiwa mdau mojawapo wa sekta ya kilimo,mifugo na uvuvi unaombwa kushiriki katika maonesho na sherehe za Nanenane ngazi ya Mkoa na Kanda kwa kuonesha bidhaa mbalimbali na teknolojia za kisasa ili kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo,ufugaji,uvuvi na maendeleo ya viwanda’’,anasisitiza Afisa Kilimo wa Manispaa.
KAULIMBIU ya Maonesho na sherehe za Nanenane 2018 ni “WEKEZA KATIKA KILIMO,UFUGAJI NA UVUVI KWA MAENDELEO YA VIWANDA”
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Julai 10,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa