MKUTANO wa Kimataifa wa wanafunzi wanasayansi vijana wa Tanzania (YST) yamefanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Juliusi Nyerere jijini Dar es salaam.Tanzania mwaka huu umeshiriki katika maonesho ya nane ya Young Sciencist Tanzania ambapo takribani wanafunzi wa shule za sekondari zaidi ya 100 kutoka mikoa yote nchini wameshiriki.
Manispaa ya Songea imetoa wanafunzi walioshiriki katika maonesho hayo ambapo washindi hupata zawadi mbalimbali ambapo washindi wa mwaka 2017 walikwenda kushiriki katika maonesho ya wanasayansi vijana nchini Afrika ya Kusini katika mji wa Durban ambako walishinda katika kundi la teknolojia.Washindi hao pia walipata fursa ya kwenda kutembelea kiwanda cha simu nchini Swedeni.
YST ni Taassisi ambayo inayojihusisha na kufadhili,kuwezesha kufanyika utafiti wa kisayansi kwa vijana katika shule za sekondari ili kuwawezesha walimu kuwasimamia wanafunzi katika utafiti ambapo mawazo ya utafiti yanatakiwa kuibuliwa na wanafunzi wenyewe.
Hata hivyo tafiti hizo za kisayansi kwa wanafunzi ni lazima zilete mawazo mapya na kutatua changamoto zilizopo katika jamii husika.Utafiti umebaini kuwa nchi ya Ireland kwa miaka kadhaa imesaidia vijana wake wanaosoma katika shule za sekondari kufanya utafiti hali ambayo imesababisha vijana wao kukuza vipaji vyao katika Sayansi na teknolojia hivyo kufika mbali katika kutumia tafiti zao ambazo zimesaidia kutatua changamoto mbalimbali katika jamii ndani ya nchi hiyo.
Naamini maonesho haya ambayo yanafanyika kila mwaka yanaweza kuleta mabadiliko makubwa kwa wanasayansi vijana wa Tanzania na kuwafikia wenzetu katika nchi nyingine ambao wamepiga hatua kubwa .
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa