HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kupitia Mpango wa Serikali wa utoaji wa Elimu bila malipo kuanzia elimu ya msingi na sekondari hadi kidato cha nne maarufu kama ‘’elimu bure‘’ imepata mafanikio yafuatayo:
Uandikishaji wanafunzi wa Elimu ya awali umeongezeka kutoka 4,834 mwaka 2015 hadi 7,242 mwaka 2018 sawa na asilimia 112 ya lengo la 6,485,Uandikishaji wanafunzi wa darasa la kwanza umeongezeka kutoka 6,475 mwaka 2015 hadi 7,661 mwaka 2018 sawa na asilimia 118 ya lengo la 6,513 na Ufaulu wa darasa la saba umeongezeka kutoka 62.4 mwaka 2015 mpaka 76.5 mwaka 2018.
Katika kipindi cha mwaka 2017/2018 hadi April 2018 Manispaa ya Songea imepokea fedha za Elimu bure jumla ya Tshs 212,123,161 kwa shule za Msingi ambapo Wanafunzi Walioripoti kidato cha kwanza wameongezeka kutoka 2,584 mwaka 2015 hadi 3,538 mwaka 2018 sawa na asilimia 73.07.Ufaulu wa kidato cha nne ni asilimia 88 mwaka 2015 na asilimia 84.9 mwaka 2018 na ufaulu wa kidato cha sita umeongezeka kutoka asilimia 97.1 mwaka 2015 hadi 98.1 mwaka 2017.
Hata hivyo Pamoja na mafanikio hayo katika elimu,Manispaa ya Songe inakabiliwa na upungufu wa Walimu wa Sayansi 95 sawa na asilimia 39.1 ikilinganishwa na Mahitaji ya Walimu 243 wa masomo hayo.
Taarifa imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Juni 16,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa