Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ina Watu Wazima 2,458 wasiojua kusoma,kuandika na kuhesabu(KKK).Afisa Elimu ya Watu Wazima Faraja Yonas amesema kati yao Wanaume ni 661 na Wanawake ni 1,797.
Kwa mujibu wa takwimu za usajili za mwezi Januari hadi Machi,Manispaa ya Songea ina jumla ya Watu Wazima 119,328,Kati yao wanaume ni 58,049 na Wanawake ni 61,279.Yonas amesisitiza kuwa Manispaa ya Songea imejipanga vizuri katika harakati za kuhakikisha watu wazima wote wanajua kusoma, kuhesabu na kuandika Kwa asilimia 100.
Anaitaja mikakati ambayo Manispaa ya Songea inachukua kutekeleza lengo la Elimu ya Watu Wazima kuwa ni kutoa elimu kwa Watu Wazima ili kuwapatia stadi za kazi muhimu kwa ajili ya
Mikakati mingine ni kuongeza ujuzi wa uzalishaji mali na kuyafahamu mazingira yao Kiuchumi, Kijamii na Kisiasa ili kuyakabili vema mazingira yao ili kufikia lengo kuu la Elimu ya Watu Wazima.
Akizungumzia kuhusu kisomo chenye manufaa na kisomo cha kujiendeleza na uzalishaji mali katika Manispaa hiyo,Yonas amesema Manispaa ina vituo 108 vya MUKEJA vyenye washiriki 2,600, wakiwemo Wanaume 937 na Wanawake 1,663.
MUKEJA ni Mpango wa uwiano kati ya Elimu ya Watu Wazima na Jamii. Katika mpango huu washiriki hujifunza mambo yanayohusu uchumi, na maendeleo ya jamii kwa ujumla, ikiwa ni pamoja na kusoma, kuandika na kuhesabu.
Katika mfumo huo Washiriki wenyewe ndiyo wanaopanga jambo la kujifunza, muda muafaka wa kujifunza, na namna ya kujifunza. Kwa maana nyingine mukeja ni Mtaala unaozingatia matakwa ya mwanakisomo katika kujifunza.
Akizungumzia kuhusu Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Watoto Waliokosa(MEMKWA),amesema mpango huo unalenga kuwapatia Elimu watoto walioikosa Elimu ya Msingi ambao wengi wao wanatoka katika mazingira magumu au familia zenye kipato duni.
Manispaa ya Songea ina vituo tisa vya MEMKWA, vyenye jumla ya wanafunzi 103 kati yao Wavulana 50 na wasichana 53.
Kulingana na Afisa Elimu ya Watu Wazima Manispaa hiyo ina jumla ya wana kisomo 154 wanaohudhuria ambapo hivi sasa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Cuba zina mpango wa kutoa Elimu ya Watu Wazima kwa kutumia Redio, Video, na Televisheni.
Imetolewa na Albano Midelo simu 0784765917
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa