MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Tina Sekambo amesema Halmashauri ya Manispaa hiyo imeanza kunufaika na mradi wa kituo cha mabasi cha Mfaranyaki ambapo ukusanyaji wa mapato umeongezeka kwa asilimia zaidi ya 300 na kwamba kodi ya vibanda pia imeongezeka toka kati ya shilingi 25,000 hadi 50,000 kwa mwezi hadi 250,000 hadi 300,000 kwa mwezi.
Sekambo amesema ongezeko hilo limetokana baada ya kufanyika ukarabati wa stendi hiyo ambao umefanya na Benki ya Dunia kupitia miradi ya ULGSP kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 550.Amesema wajasirimali wakubwa na wadogo wamevutiwa kufanya biashara katika kituo hicho kutoakana na kuwa na mazingira rafiki ya biashara.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa