MKUU wa Idara ya Maji katika Manispaa ya Songea Mhandisi Samwel Sanya anasema Idara ya maji inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali chini ya mpango wa maendeleo ya sekta ya maji awamu ya kwanza (WSDP I) ambapo Halmashauri ilitekeleza miradi katika mitaa tisa kwa asilimia 100 iliyogharimu jumla ya Tshs. 1,656,786,632.
Hata hivyo amebainisha kuwa miradi ya Mitendewawa na Luhilakati imekamilika kwa asilimia 80 ambapo watu 4141 wanapata huduma.
Kulingana na Mhandisi Sanya,Katika mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri ya Manispaa ya Songea katika bajeti yake imepanga kujenga miradi ya visima vya maji 90 katika mitaa 15 na kwamba hadi sasa miradi katika mitaa hiyo ipo katika hatua tofauti tofauti ya utekelezaji itakayo hudumia wananchi 22,500.
Amesema Katika mwaka wa fedha 2017/2018 zimepokelewa jumla ya shilingi 485,387,405.00 na kwamba Hadi kufikia mwezi Juni 2018 jumla ya Tshs. 389,811,424.00 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji katika mitaa ya Mitendewawa na Ruhilakati.
Hata hivyo amesema hali ya upatikanaji wa huduma ya maji pembezoni mwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea ni asilimia 46.6
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa