HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ina fursa na vivutio vingi vya utali ambavyo husababisha matukio mbalimbali ya shughuli za utalii na za kiutamaduni kufanyika kama vile, Tamasha la Kitaifa la kumbukizi la vita vya majimaji linalofanyika kila mwaka kuanzia 25 Februari mpaka tarehe 27 Februari ambayo ni siku ya kilele na ni siku ambayo walinyongwa mashujaa wa vita vya majimaji,
Matamasha mengine ambayo hufanyika kila mwaka katika Manispaa ya Songea ni tamasha la Majimaji Serebuka linaloendeshwa na NGO’s ya Songea Mississippi shughuli zinazofanyika ni maonesho ya ujasiliamali, mashindano ya ngoma za asili, study tour, mbio za marathoni, mbio za baiskeli, fiesta na maonesho ya mashujaa wa vita vya Kagera.
Halmashauri ya Manispaa ya Songea ina hifadhi moja ya wanyamapori ambayo ni hifadhi ya Ruhira (Ruhira game reserve) inayosimamiwa na Kikosi cha kuzuia ujangili kanda ya kusini (KDU) chini ya Mamlaka ya Kusimamia Wanyamapori Tanzania (TAWA)
Kazi kubwa ya sekta ya wanyama pori ni kulinda na kuhimiza ulinzi wa wanyama pori ambao ni hazina ya nchi yetu. Vilevile ni jukumu la sekta kulinda na kuendeleza hifadhi ya wanyamapori katika pori la akiba Ruhira, Kulinda mali na maisha ya wananchi kutokana na wanyama wakali na waharibifu, na uhamasishaji, uhifadhi na ulinzi wa wanyamapori katika mitaa inayozunguka pori pamoja na kufanya doria kwa kuzuia ujangili.
Halmashauri ya Manispaa ya Songea ina jumla ya misitu ya hifadhi 10, kati ya hiyo misitu mitatu (West Matogoro 1000.5ha, East Matogoro 7457.24ha na South Matogoro 6755.7ha) ni ya Serikali Kuu inasimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) na misitu 7 (Likuyu 722ha, Kwalikucha 33ha,Namanyigu 7.1ha,Chandamali 29ha,Liumbu 66.8ha na Unangwa 20ha, Nangwai 72.9ha)
Halmashauri kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mazingira imepanda jumla ya miti 925,146 katika Misitu ya hifadhi Matogoro, vyanzo vya maji vya bonde la mto Ruhila na milima ya Kwalikucha-Liwena ilitoa jumla ya kilogramu 112 za mbegu za miti na viriba kilogramu 200. Aidha halmashauri ina mizinga 1040 ya ufugaji Nyuki inayomilikiwa na vikundi,taasisi na ya watu binafsi. Hali hii inasaidia kuboresha vyanzo vya maji,kuboresha mazao ya misitu na zao la asali ambapo litasaidia kuongeza kipato cha wananchi.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari wa Manispaa ya Songea
Septemba 17,2018.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa