DIRA ya Maendeleo ya Manispaa ya Songea ni kuwa kitovu cha uwekezaji na Mji wa viwanda kwa kutoa huduma bora na endelevu kwa lengo la kuinua maisha ya wananchi.
Dira hiyo inakwenda sanjari na na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya hadi mwaka 2025.Dira hiyo inalenga kupunguza umaskini uliokithiri miongoni mwa wananchi.
Kutokana na Dira ya Halmashauri yetu na ile ya Taifa ya mwaka 2025,Manispaa ya Songea inatekeleza mpango wa kupunguza umaskini unaozingatia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa CCM ya mwaka 2015.
Shughuli muhimu za kiuchumi katika Manispaa ya Songea ni kilimo na biashara.Kilimo huchangia asilimia 75 ya pato lote la Halmashauri ambapo mazao yanayowapatia mapato makubwa wananchi wa Manispaa ni mpunga na mahindi.
Kutokana na shughuli hizo za kiuchumi pato la wananchi ni wastani wa sh.738,002 kwa mwaka hata hivyo lengo la Manispaa ni kuhakikisha pato la mtu linaongezeka hadi kufikia sh.milioni moja kwa mwaka ifikapo mwaka 2020.
Manispaa ya Songea inakadiriwa kuwa na idadi ya watu 260,106 wakiwemo wanaume 124,340 na wanawake 137,171 kutokana na ongezeko la asilimia 4.4 kwa mwaka.Manispaa ya Songea yenye mitaa 95 na kata 21 ina jumla ya kaya 61,930 kwa wastani wa watu 4.2 katika kila kaya.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa