Halmashauri ya Manispaa ya Songea inatarajia kufanya uzinduzi wa kampeni ya jiongeze tuwavushe salama wiki ijayo inayolenga akina mama wajawazito Mkoani Ruvuma.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Dkt. Mameritha Basike amesema mgeni rasmi katika uzinduzi huo utakaofanyika katika Kata ya Ruvuma, anatarajia kuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema.
Kulingana na Dkt.Basike azma ya kuzindua kampeni hiyo ni kutekeleza kampeni hiyo ni kuwafanya wananchi, watendaji wa serikali,wanasiasa na viongozi wa dini kufahamu afya ya mama na watoto kuwa ndiyo agenda kuukatika Halmashauri ili kupunguza na kutokomeza kabisa vifo vya akina mama nawatoto chini ya miaka mitano.
Basike amebainisha kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea ni miongoni mwa Hamashauri zinazokumbwa na tatizo la vifo vya akina mama na watoto ambapo ameitaja Kata ya Ruvuma kuwa inaongoza kwa vifo vya akina mama na watoto kwa Mwaka 2018 ambapo imeripotiwa vifo vya watoto 36, akina mama watatu
Na akina mama wanaliojifungulia nyumbani ni 32.
Basike ameongeza kuwa uzunduzi huo umepangwa kuzinduliwa katika Kata ya Ruvuma na ametoa wito kwa jamii kuhudhuria ili kuweza kufahamu masuala mbalimbali yanayohusu afya ya mama na mtoto kwa kuwa itatolewa elimu itakayohamasisha akina mama umuhimu wa kuhudhuria klinikina kuhakikisha wanajifungua hospitalini au katika vituo vya afya.
“Zitungwe sheria ndogondogo zitakazotumika kuwaadhibu wasiohudhuria clinic, Baba au Mama akamatwe na ikiwezekana atozwe faini.”Amesema Basike.
Katika hatua nyingine Dkt. Basike ameiomba jamii kujiunga na huduma ya CHF iliyoboreshwa ili waweze kupata matibabu katika vituo mbalimbali vya afya kwa gharama nafuu zaidi katika Manispaa ya Songea,
Sanjari na hilo Dkt.Basike ametoa rai kwa jamii kwa wanajamii kuwatambua wakunga wa jadi waliostaafu ili waweze kuwapatia elimu ya uzazi na kuthamini mchango wa wazee maarufu (mila).
Imeandikwa na
Bacilius Kumburu
Wa kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Agosti 9, 2019.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa