HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imeendelea kufanya vizuri katika matokeo ya shule za msingi na sekondari baada ya kufaulisha kidato cha sita kwa asilimia 99.
Afisa Taaluma Sekondari wa Manispaa hiyo Osimund Mkinga amesema matokeo hayo yameifanya Halmashauri hiyo kuongoza katika Mkoa wa Ruvuma kati ya Halmashauri nane zilizopo na kwamba kitaifa Mkoa wa Ruvuma umeshika nafasi ya sita kati ya mikoa 26 ya Tanzania bara.
“Sisi kama Idara ya Elimu katika Manispaa ya Songea tumejipanga kuhakikisha tunawahamasisha walimu ili kuendelea kufanya vizuri katika kidato cha nne na cha sita’’,alisisitiza Mkinga.
Kulingana na Mkinga katika matokeo ya kidato cha sita kitaifa mwaka 2017 Manispaa hiyo ilifaulisha kwa asilimia 87.6 na kushika nafasi ya 76 kitaifa na kwamba katika mwaka huu 2018 Manispaa ya Songea kitaifa imepanda hadi kushika nafasi ya 46.
Manispaa ya Songea ina jumla ya shule za sekondari 40 za kidato cha nne kati ya hizo sekondari 24 ni za serikali na 16 za binafsi na kwamba shule tano za kidato cha sita kati ya hizo mbili za serikali na tatu za binafsi.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Julai 22,2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa