Manispaa ya Songea yakamata vipodozi vyenye sumu
IDARA ya Afya katika Manispaa ya Songea imefanikiwa kukamata vipodozi na vyakula vyenye sumu vikiwa na thamani ya zaidi sh.milioni mbili.
Vipodozi hivyo vimekamatwa katika kipindi cha kuanzia Aprili hadi Juni mwaka huu katika ukaguzi endelevu ambao unafanywa na Idara hiyo.
Baadhi ya vipodozi vyenye sumu ambavyo vimekamatwa kuwa ni actif plus, betasol, broze, cocoderm, carolight, carotone, citrolight,clairmen,cocopulp,corton,diproson na epiderm.
Vipodozi vingine ni,extralair,jaribu,lemonvate na mekako, miki, Montclair, movate, Naomi, oranvategel, perfect, princes, rapid, sabuni protex,seven mirackes, toplemon, whiteplus, dodo, teint, superclair,greeting,14 days, dermotyl, natural,gold touch,coco dermbetacort,extral white, fomura avas, lemon cream na diva maxmum.
Katika ukaguzi huo pia vimenaswa vipodozi halali ambavyo vimemalizika muda wake vyenye thamani ya zaidi ya sh.500,000.Vipodozi vilivyomalizika muda wake ni skin soft,pure glycerine,royal touch,u&me na mambo fresh.
Katika kipindi hicho Idara hiyo pia imekamata vyakula vilivyokuwa vinauzwa wakati muda wake umekwisha vyenye thamani ya zaidi ya sh.300,000.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa