HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imefanikiwa kukusanya mapato kwa asilimia 81 katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2017/2018.Akizungumza kwenye mkutano wa kufunga mwaka wa Baraza la madiwani la manispaa hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Alto Liwolelu amesema tofauti ya makusanyo ni asilimia 19 na kwamba kodi za viwanja ndizo ambazo zimekwamisha makusanyo hayo hali ambayo imesababisha Manispaa hiyo kushindwa kufikia malengo ya kukusanya kwa asilimia 100.
Hata hivyo amesema masoko hayo hayafanyi kazi ndiyo yamekwimisha manispaa hiyo kushindwa kufikia malengo na kwamba katika manispaa hiyo kuna masoko manne ambayo hayafanyikazi na chanzo chanzo cha makusanyo katika viwanja yalikuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 400 ambapo katika kikao cha Kamati ya Fedha na Uongozi wamekubaliana kuhakikisha kuwa changamoto zilizopo katika masoko hayo zinatafutiwa ufumbuzi ili yaweze kuanza kufanyakazi na kwamba manispaa inatarajia kuwatambua wafanyabiashara wote kwa kuwapa vitambulisho ili wasikwepe kulipa ushuru.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Alhaj Abdul Hassan Mshaweji ameyataja malengo ya Manispaa hiyo katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2018/2019 ni kuhakikisha kuwa mapato ya manispaa ya Songea yanakusanywa kwa asilimia 100 na kuzuia mianya yote inayosababisha mapato kuvuja na kwamba Manispaa imejipanga kubuni vyanzo vipya vya mapato hali ambayo itawezesha manispaa hiyo kufikia malengo yaliyokusidiwa.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Agosti 6,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa