HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imepata Hati safi katika mwaka wa fedha wa 2016 /2017 baada ya ukaguzi uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Manispaa ya Songea kufanya vizuri ambapo katika mwaka wa Fedha wa 2015/2016 ilipata Hati inayoridhisha.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG ) Profesa Musa Juma Assad pia ameridhika pasipo mashaka kuwa Sheria ya Manunuzi Namba Saba ya mwaka 2011 na kanuni za mwaka 2013 zilifuatwa ipasavyo katika michakato yote ya Manunuzi yalifanyika kwa mwaka 2015/2016 na mwaka 2016/2017 kwenye manispaa ya Songea.
Halmashauri ya Manispaa ya Songea ni moja kati ya Halmashauri nane za Mkoa wa Ruvuma ikiwa na tarafa mbili, kata 21 na mitaa 95.
Taarifa imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa