Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Ahmed Abbas Ahmed amewataka wataalamu wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kuacha matumizi ya fedha mbichi (Matumizi mabaya ya fedha).
Kauli hiyo imetolewa kupitia baraza maalum la Madiwani la kujadili taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) juu ya hoja ya mapendekezo ya CAG hesabu za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Akisoma hotuba hiyo Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bi Rehema Madenge kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma aliwapongeza wataalamu wa Manispaa ya Songea pamoja na Madiwani wote kwa kupata HATI SAFI.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu kwa hesabu za fedha kwa mwaka 2022/2023 zimetolewa hoja namapendekezo 33 ambapo hoja zote zenye kustahili kufungwa zitafutiwe majibu na vielelezo vinavyotakiwa kuwekwa kwenye taarifa na kufungwa hoja hizo kabla ya tarehe 30 Septemba na taarifa ya utekelezaji wa hoja hizo zipelekwe ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
Alisema, Manispaa ya Songea iendelee kupata hati safi kwa miaka miwili ijayo mambo muhimu yanahitaji kuzingatia ambayo ni hakikisheni hoja zote zinafungwa, Kuzuia hoja zisizo za lazima, Wakuu wa Wilaya washirikishwe wakati wa kujibu Hoja, kuchukua hatua za haraka kwa watumishi wanaosababisha hoja kizembe, Afisa Mashuhuri ashiriki kikao cha Hoja bila kukaimisha, Hesabu za mwaka kupitia Benk satatment ziaandaliwe mapema, Fedha zote zinazokusanywa zihakikishwe zinawekwa benk na zitoke kwa utaratibu Maalmu ndipo zianze kutumika ( Fedha Mbichi).
Aidha, Halmashauri iendelee kulipa madeni mablimbali ya zabuni kwa wakati, vikao vya ugazi viendelee kufanyika kwa wakati, kufuatilia vikao vya wadaiwa sugu kupitia vikundi vya wananwake, vijana, na walemavu ambao bado hawajarejesha mikopo yao, kufuatilia huduma ya CHF iliyoboreshwa, Hakikisha mfumo wa GOTHOMISI unafungwa katika vituo vya afya, Wataalamu na Madiwani kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili uendane na thamani ya fedha kwa wahasibu wazembe wenye kuleta ubadhilifu, kulipa satahiki za watumishi wanazodai, Maelekezo yote ya LAAC yatekelezwe na yafungwe kabla ya kufika vikao vya Serikali za Mitaa.” Amesisitiza “
Kwa upande wake Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali CPA Deogratias Waijaha amewapongeza Manispaa ya songea kwa kupata HATI SAFI, pia amewataka wataalamu hao kufanya kazi kwa weredi kuondoa hoja mbalimbali za kushindwa kukusanya mapato ya vibanda vya Halmashauri pia kuhakikisha wanaondoa madeni ambayo Halmashauri imekuwa ikidai madeni zaidi ya Bil 1.6 pia Manispaa ilikuwa ikidaiwa Mil 485 ambapo amewataka kuendelea kukusanya madeni hayo na kulipa kwa wanaowadai.
Akizungumza Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Mhe. Michael Mbano amewataka wataalamu kuhakikisha wanaweka mikakati ya kuondoa hoja za ukaguzi na sio kuwa walimu wa kujibu wa hoja.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa