KUPITIA Mpango wa Elimu bila malipo katika shule za msingi za Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa mwaka wa fedha 2016/2017 imepokea zaidi ya milioni 616.812 na Kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri hadi kufikia Juni imepokea zaidi ya 613.
Upatikanaji wa fedha hizi umeboresha miundombinu ya madarasa, vyoo, samani, upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia mashuleni na hivyo kufanya kazi ya ufundishaji kuwa rahisi kwa Walimu sawa na asilimia 100 ya utekelezaji wa fedha zilizopokelewa za Elimu Bila malipo.
Kutokana na ongezeko la usajili wa wanafunzi kwa sasa halmashauri ina upungufu wa madawati 1002. Hata hivyo ili kukabili upungufu huo kwa mwaka huu wa fedha 2018/2019 Halmashauri imetenga zaidi ya shilingi milioni 35.569 Kwa ajili ya kutengeneza madawati 547.
Manispaa ya Songea kwa mwaka wa fedha 2016/2017 na 2017/2018 imepokea fedha ya mradi wa Lipa kulingana na matokeo (P4R) jumla ya shilingi milioni 415,100,000.00.Kutokana na Mpango wa elimu bure,ufaulu wa wanafunzi kwa darasa la saba umetoka asilimia 64.4 mwaka 2015 na kufikia asilimia 76.5 mwaka 2017.
Hata hivyo taarifa ya Idara ya Elimu Msingi Katika mwaka 2018 inaonesha kuwa jumla ya wanafunzi wawili walibainika na kuripotiwa kuwa na mimba na kwamba hali ya utoro imepungua kutoka asilimia 0.5 mwaka 2016 hadi asilimia 0.4 mwaka 2017
Halmashauri ya Manispaa ya Songea ina jumla ya Shule za Msingi 89 na Madarasa ya Awali 89 ambayo yapo katika kila Shule ya Msingi. Shule hizi zina darasa la Awali hadi darasa la saba zikiwa na jumla ya wanafunzi 54131 kati yao wavulana 26,785 wasichana 27,346.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Septemba 10,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa