Pamoja na changamoto mbalimbali za sekta ya Afya, Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,Manispaa hiyo imefanikiwa kupunguza maambukizi ya UKIMWI kutoka asilimia 3.9 mwaka 2017 hadi asilimia 3.2 mwezi machi 2018.
Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Dk.Mameritha Basike amesema huduma za Afya ya uzazi na mtoto zinatolewa katika vituo 29 na kwamba huduma zinazotolewa ni chanjo kwa Watoto chini ya mwaka mmoja, huduma kwa wajawazito na wazazi ili kuzuia maambukizi ya Ukimwi toka kwa Mama kwenda kwa Mtoto ikiwemo ushiriki wa akina Baba.
Hata hivyo Dk.Basike amesema vifo vya Wajawazito bado ni tatizo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa sababu takwimu zinaonesha kuwa vifo hivyo vimeongezeka toka 182/10000 Mwaka 2016 hadi vifo 202/100,000 mwaka 2017 ambapo jitihada za kupunguza vifo hivyo vya akina mama zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuimarisha huduma za upasuaji katika kituo cha Afya cha Mjimwema.
Kulingana na Mganga Mkuu huyo wa Manispaa ya Songea,Magonjwa yanayoongoza katika Manispaa ni Malaria kwa asilimia 34,magonjwa ya mfumo wa hewa asilimia 32.3,magonjwa ya njia ya mkojo(UTI) kwa asilimia 11.2,Magonjwa ya ngozi kwa asilimia 9.9,Magonjwa ya vichomi(Nimonia) asilimia7.6 na magonjwa ya kuhara asilimia 5.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Agosti 20,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa