JUMLA ya vikundi 45 vya wajasirimali wadogo kutoka katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma vimepewa mikopo ya jumla ya shilingi milioni 85.Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Manispaa hiyo Naftari Saiyoloi akitoa taarifa katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea amesema Kati ya vikundi hivyo,vikundi vya wanawake ni 21 vilivyokopeshwa shilingi milioni 28, kundi la wenye ulemavu wamepewa shilingi milioni 15 na vikundi 14 vya vijana vimekopeshwa shilingi milioni 20.
Hata hivyo amesema katika robo ya pili ya mwaka 2019/2020 kutokana na mapato ya ndani ya asilimia 10,Idara imepewa shilingi milioni 30 ambapo kwenye marejesho zimetolewa shilingi milioni 40 na kwamba Manispaa ya Songea imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mikopo hiyo inatolewa kwa mujibu wa sheria.
Naye Mgeni rasmi katika hafla hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema akizungumza katika hafla hiyo ameipongeza Manispaa ya Songea kwa kuwa mstari wa mbele kutoa mkopo wa fedha za mapato ya ndani kwa asilimia kumi kwa vikundi vya wajasirimali ambapo ameviagiza vikundi hivyo kuhakikisha kuwa fedha walizokopeshwa wanazirejesha ili zitumike kukopesha wengine.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa