HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma inaendelea kunufaika kupitia fedha za ULGSP ambapo mwezi huu imeweza kununua viti maalum aina ya Airport sit zenye thamani ya shilingi milioni 1.4 ambavyo vimesambazwa katika Idara zenye wateja wengi wanaofika kupata huduma katika ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Afisa Utumishi wa Manispaa ya Songea Buruani Mapunda amesema Halmashauri imeamua kununua viti hivyo ili kupunguza usumbufu wa wateja kusimama wakati wanasubiri kupata huduma.Ofisi ambazo zimepewa viti hivyo kuwa ni Idara ya Utumishi,kitengo cha Biashara na ardhi.Halmashauri ya Manispaa ya Songea ni miongoni mwa Halmashauri 18 nchini ambazo zipo katika mradi wa ULGSP.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa