MANISPAA YAFAULISHA KWA ASILIMIA 97
HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imeendelea kufanya vizuri katika mtihani wa Taifa wa kidato cha sita baada ya kufaulisha kwa asilimia 97.2.Kwa mujibu wa matokeo hayo,katika shule tano za serikali za kidato cha sita wanafunzi waliopata daraja la kwanza ni 62 kati yao wavulana ni 34 na wasichana ni 28.
Daraja la pili lina jumla ya wanafunzi 471 kati yao wavulana ni 174 na wasichana 297,daraja la tatu jumla ya wanafunzi 507 kati yao wavulana ni 179 na wasichana 328.Kulingana na matokeo hayo,daraja la nne lina jumla ya wanafunzi 47 kati yao wavulana 23 na wasichana 24 na waliopata daraja sifuri ni 24 kati yao wavulana 10 na wasichana14.Shule za serikali ambazo zimefaulisha wanafunzi hao ni sekondari ya wavulana Songea,sekondari ya wasichana Songea, Msamala, Londoni na sekondari ya Emanuel Nchimbi.
Matokeo ya kidato cha sita kwa shule mbili ambazo sio za serikali yaani sekondari ya Beroya na Ruhuwiko yanaonesha kuwa jumla ya wanafunzi wanne walipata daraja la kwanza na wanafunzi 98 wamepata daraja la pili.Wanafunzi waliopata daraja la tatu katika shule hizo ni 105,daraja la nne wanafunzi wanne na mwanafunzi mmoja tu amepata daraja sifuri.Manispaa ya Songea ina jumla ya shule saba zenye kidato cha sita.
Taarifa imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari wa Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa