MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Tina Sekambo amesitisha uchinjaji wa nguruwe katika maeneo yote ya Manispaa hiyo kufuatia kuibuka kwa homa ya nguruwe.
Katika kipindi cha wiki mbili homa ya nguruwe(African Swine Fever) imeua nguruwe zaidi ya 120 hali ambayo inataharisha kuteketeza nguruwe katika Manispaa hiyo ambapo takwimu zinaonesha kuwa Manispaa hiyo ina jumla ya nguruwe 4581.
Kutokana na kuenea kwa Homa ya Nguruwe (African swine fever) katika Manispaa na ili kuzuia usambaaji zaidi wa Homa ya Nguruwe,Mkurugenzi anaagiza watendaji wote wa Mitaa na Kata kuanzia sasa wahakikishe hakuna mtu, kuchinja nguruwe, kusafirisha nguruwe (kuingia au kutoka) na mazao yake katika maeneo ya Manispaa
Daktari wa Mifugo katika Manispaa hiyo Erick Kahise anasema katazo hili litasaidia kusiwe na uwezekano wa watu kusafirisha nguruwe kwa namna yeyote ile na vifo vyote na taratibu za unyunyiziaji kufanyika katika kila eneo.
Manispaa ya Songea ina jumla ya mitaa 95 na kata 21,maeneo ambayo yanaongoza kwa homa hiyo ni kata ya Lizaboni ambayo nguruwe zaidi ya 100 wamekufa,kata nyingine ni Mjimwema, Mshangano na Ruhuwiko.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Februari Mosi,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa