HALMASHAURI ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imekuwa na utaratibu wa kuwezesha vikundi vya Wanawake na Vijana kujiongezea kipato kwa kukopeshwa kutoka katika fedha za mapato ya ndani.
Kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kwa kutumia mapato ya ndani Halmashauri ya Manispaa ya Songea ilitoa jumla ya shs. 88,800,000.00 ambazo zilikopeshwa vikundi 128 vyenye wanufaika 1992, kati ya hao wanawake ni 1394 na vijana 598, vikundi vya wanawake 82 vilikopeshwa shs.59,800,000.00 na vikundi vya vijana 46 vilikopeshwa shs. 29,000,000.00 na hadi kufikia mei, 2018 marejesho ya mkopo huu ni jumla ya shs. 50,000,000.00
Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2017/2018 Halmasahuri ya Manispaa ya Songea ilipanga kutumia jumla ya shilingi 169,768,620.00 kwa ajili ya Kukopesha vikundi 100 vya wanawake na vikundi 77 vya vijana.
Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa kipindi cha Julai, 2017 hadi Machi 2018 ilikopesha jumla ya shs. 116,000,000.00 kwa jumla ya vikundi 102, vyenye wanufaika 1,323 vikundi vya wanawake 87 vilikopeshwa shs. 101,100,000.00 wanufaika 1,131 na vikundi vya vijana 15 vilikopeshwa shs. 14,900,000.00 wanufaika 192.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka huu Charles Kabeho akiwa katika Manispaa ya Songea amezindua utoaji wa Mkopo wa shs. 60,000,000.00 ambao ulitolewa kwa vikundi 32 vya Wanawake shs.44,000,000.00 vyenye wanufaika 461 na Vikundi 10 vya Vijana shs. 16,000,000.00 vyenye wanufaika 187 na kufanya jumla ya wanufaika 648, ambao wamekwisha patiwa mafunzo ya ujasiriamali na maelekezo ya urejeshaji wa mikopo hii.
Taarifa imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Juni 14,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa