WATOTO mapacha walioungana Maryness na Anisia Beatusi, wamepelekwa nchini Saudia Arabia kwa matibabu baada ya kupata ufadhili kutokana na uhusiano mzuri baina ya Serikali ya Tanzania na nchi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Balozi wa Saudia Arabia nchini Mohammed El Malik amesema Mfalme wa Saudia amewafadhili watoto hao baada ya ombi lilitolewa na Serikali ya Tanzania.
Akizungumzia upasuaji huo Daktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Petronila Ingiloi amesema kuwa wamepata ugumu hasa kwenye matokeo ya mwisho baada ya kufanikisha upasuaji wa watoto hao.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji watoto, Zaituni Buhari ambaye anasafiri na watoto hao amesema uchunguzi wa awali utafanywa kwa umakini ili kuweza kufanikisha upasuaji salama kwa watoto hao.
Chanzo cha habari hii ni https://www.malunde.com/2018/07/mapacha-walioungana.html
USISAHAU KUTEMBELEA TOVUTI YETU KILA SIKU songeamc.go.tz
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa