MASALIO ya aina tatu za mijusi ambayo inaaminika iliishi miaka milioni 240 iliyopita yamegundulika katika Pori la Akiba la Litumbandyosi,Bonde la Ruhuhu wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.
Afisa Maliasili na Utalii wa Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe anasema ugunduzi huo licha kuongeza vivutio vya utalii katika Pori la Akiba la Litumbandyosi,lakini pia unaongeza vivutio vya utalii katika Mkoa wa Ruvuma hali ambayo itafungua milango ya utalii.Masalia ya mabaki ya mijusi hiyo,yamegundulika katika maeneo ya Manda,Lifua,Kingori na Usili ndani ya Bonde la Ruhuhu na kwamba masalia ya mijusi inaaminika imeishi miaka mingi zaidi duniani ukilinganisha na aina nyingine za masalia ya mijusi
Ugunduzi wa masalia mengine ya mijusi katika Bonde la Ruhuhu mkoa wa Ruvuma yanafungua milango ya utalii katika ukanda wa kusini wenye mikoa ya Ruvuma,Lindi na Mtwara.Wanasayansi waliogundua,aina tatu za masalia ya mijusi bonde la Ruhuhu wanazitaja aina hizo kuwa ni ruhuhuensis iliyogunduliwa katika eneo la Kingori, ruhuhuaria ambayo imegundulika eneo la Manda Lifua na masalia ya mijusi aina ya ruhuhucerberus eneo la Kawinga.
Mgunduzi wa masalia ya mijusi ya ruhuhuaria anaitwa Fransis Perrington ambaye anaaminika aliyagundua kwa mara ya kwanza mwaka 1930 katika miamba tabaka ya Lifua Manda Bonde la Ruhuhu.Masalia ya mjusi aina ya Ruhuhucerberus yaligundulika eneo la Kawinga mwaka 2002 na masalia ya awali ya mijusi ya Ruhuhuensis iligundulika mwamba wa Usili Bonde la Ruhuhu mwaka 1950.
Hata hivyo Utafiti wa mwisho kuhusiana na masalia ya mijusi hiyo ulifanyika kati ya mwaka 2007 na 2008 na Timu ya watafiti toka nchi za Uingereza na Marekani na kugundua idadi kubwa ya masalia ya mijusi hiyo katika Bonde la Ruhuhu.
Watafiti hao wa kimataifa wa Makumbusho,wakioongozwa na Ken Angielzyk na Bill Simpson walikuwa ni miongoni mwa wanasayansi wa kimataifa waliofika Bonde la Ruhuhu kufanya uchunguzi na kufanikiwa kukusanya idadi kubwa ya masalia ya mijusi ambayo inaaminika iliishi miaka mingi zaidi duniani.
“Masalia haya ya mijusi jamii ya mamba yalijadiliwa katika nyaraka (Thesis) kadhaa katika chuo kikuu cha Cambridge,Uingereza,inakadiriwa kwamba jamii hiyo ya mijusi iliishi bonde la Ruhuhu miaka milioni 240 iliyopita’’,anasema Afrikanus Challe Afisa Maliasili na Utalii wa Mkoa wa Ruvuma.
Kulingana na vipimo vya kiikolojia kwenye mabaki ya mijusi hiyo,inaaminika dinosaurs wa Bonde la Ruhuhu ana urefu wa meta kati ya 2.7 hadi 10,ana shingo ndefu na mkia, na alikuwa na miguu minne kama mamba.
Challe anasema ugunduzi wa masalia ya mijusi katika bonde la Ruhuhu ni mafanikio makubwa kwa wanasayansi hao kwa sababu wamegundua kile wanachoita kama ni chanzo cha kizazi cha dinosaurs na kwamba ugunduzi huo mpya umejaza pengo kubwa katika historia ya mabaki ya mjusi huyo adimu duniani.
Tanzania imebahatika kuwa na masalia ya viumbe adimu duniani ambavyo vinavutia watalii kila kona hapa nchini kufika kufanya tafiti na kutembelea katika maeneo husika.Moja ya vivutio hivyo ni masalia ya mjusi ambaye anafahamika kwa jina la Tendaguru anayepamba makumbusho ya Ujerumani ambaye masalia yake yaligundulika mkoani Lindi.
Masalia ya mjusi huyo yalivumbuliwa katika eneo la Tendaguru wilayani Kilwa mkoani Lindi zaidi ya miaka 100 iliyopita.Mjusi huyo ni kuvutio adimu katika Makumbusho ya Berlin nchini Ujerumani ambaye ana uzito wa tani 50.Mjusi huyo anakadiriwa kuwa na umri wa miaka milioni 150,ana urefu wa meta 13.7 kwenda juu,anakadiriwa kuwa na moyo wenye uzito wa kilo 400 na chakula cha mjusi huyo kilikuwa ni m
Mwandishi wa makala haya ni Albano Midelo,mawasiliano albano.midelo@gmail.com,simu 0784675917
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa