MKUU wa Majeshi ya Ulinzi na usalama nchini Generali Venance Mabeyo amesema mashujaa 67 wa vita ya Majimaji walionyongwa kikatili na wakoloni wa kijerumani mwaka 1906 walikuwa na uzalendo wa kweli na nchi yao ndiyo maana walijitolea hadi kufa kwa ajili ya ukombozi wa wananchi.
Generali Mabeyo ameyasema hayo wakati ànazungumza na wananchi wa Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma katika kilele cha kumbukizi ya miaka 113 ya mashujaa wa Majimaji yaliofanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji ambapo Mkuu huyo wa majeshi alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za mwaka huu.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa