Halmashauri ya Manispaa ya Songea ina jumla ya Mitaa 94 iliyopo katika kata 21 zilizopo ndani ya Manispaa ya Songea. Kwa mujibu wa orodha ya Mitaa iliyotangazwa kupitia gazeti la Serikali tarehe 06 Septemba 2024, tangazo hili limetangaza majina na mipaka ya Mitaa kwa ajili ya uchaguzi wa Wenyeviti wa Mitaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Tangazo hilo lilitolewa na Msimamizi wa Uchaguzi Manispaa ya Songea, Wakili Bashir Muhoja, tarehe 16 Septemba 2024. Hii ni kwa lengo la kuhakikisha uwazi na usahihi katika mipaka ya Mitaa kabla ya uchaguzi. Msimamizi huyu anatekeleza mamlaka aliyopewa chini ya kanuni Namba 5 ya Kanuni ya Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa 2024, kama ilivyoainishwa katika Tangazo la Serikali Namba 574 la tarehe 15 Agosti 2024.
Matangazo haya yalifanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea na yalihusisha vyama vya siasa pamoja na wasimamizi wa uchaguzi wa Manispaa ya Songea.
Imeandaliwa na:
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa