MBEGA adimu duniani ambao kitaalam wanaitwa Black and white colubus wameonekana wiki hii kwenye misitu ya Kilangajuu wilayani Mbinga Mkoa wa Ruvuma, wanyama hao ambao katika ukanda wa kusini wanapatikana wilayani Mbinga Mkoa wa Ruvuma wameshuhudiwa na Mhifadhi Mstaafu wa Wizara ya Maliasili na utalii Ngwatura Ndunguru ( pichani aliyeshika kiona mbali)ambaye pia ni mkazi wa Kijiji cha Kilangajuu. Wanyama hao wanapatikana kaskazini mwa Tanzania katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha.Katika wilaya ya Mbinga wanyama hao walikuwa wanapatikana katika msitu wa Liwilikitesa,hata hivyo kutokana na wawindaji kuwashambulia, wanyama hao wapo katika hatari ya kutoweka. Ndunguru anasema aliwaona wanyama hao mara ya mwisho katika msitu wa Liwilikitesa mwaka 1973 akiwa Afisa wanyamapori wa Mkoa wa Ruvuma .Anasema tangu mwaka 1973,,licha ya kuwatafuta kwa miaka mingi, ndiyo amebahatika kuwaona wanyama hao mwaka huu.Ni vema Idara ya Maliasili na utalii kufanya utafiti ili kubaini idadi kamili ya wanyama hao ambao wapo katika hatari ya kutoweka Duniani.Mnyama huyo ambaye anaponzwa na uzuri wa sura yake ana tabia ya kuzaa mtoto mmoja.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa